Mpango wa Serikali wa kunusuru kaya maskini umeendelea kunufaisha walengwa wa TASAF Wilayani Kwimba ambapo zaidi ya shilingi milioni 365.1 zimelipwa kwa kaya 7892 mwezi Julai, 2021.
Katika zoezi hilo la ugawaji wa fedha kwa kaya maskini,malipo ya mwezi Machi na Aprili walengwa wamepata nafasi ya kutoa maoni jinsi fedha hizo zinavyowasaidia katika maisha yao "nashukuru Serikali kwa kuendelea kutupatia hela za kutusaidia kununua Chakula, vifaa vya wanafunzi kwa sababu kupitia hizi hela watoto wetu wanapata madaftari, sale za Shule na familia tunajikomboa kwa kuanzisha ufugaji ambapo nimefika mbuzi na kuku ili dhamani ya fedha hizo iendelee kuonekana" amesema Biedile Lupondola.
Aidha Mratibu wa TASAF (W) Bi. Celestina Mushi amesema zoezi la utoaji fedha kwa walengwa wa TASAF limefanyika vizuri na Elimu inatolewa kwa walengwa kabla hawajapewa fedha ili kuwahamasisha wapato fedha hizo watumie kiasi kwa ujasiriamali kama ufugaji na kazi nyingine zitakazowasaidia kuendelea kupata kipato.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.