Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija aendelea kutembelea Kata kwa Kata kusikiliza malalamiko na kero za wananchi.
Katika kuendeleza utaratibu huo Leo Septemba 26,2023 Mheshimiwa Ludigija amesikiliza kero za wananchi wa Kata ya Nyamilama na maeneo jirani na kero za wananchi wa Hungumalwa.
Mkuu huyo amefanya ziara hiyo akiwa ameambatana na wataalamu wa idara mbalimbali kama maji, Tanesco, Halmashauri, Tarura na wataalamu wengine ambao wamejibu na kutoa ufafanuzi wa malalamiko na kero zilizojitokeza.
Katika ziara hiyo kero zilizojitokeza ni upatikanaji wa maji, huduma ya umeme vijijini kutowafikia wananchi wengi, Barabara kutokarabatiwa kwa wakati, na ukosefu wa elimu na uelewa juu ya namna ya kulipa ushuru wa mazao kwa wanaofanya biashara ya mazao.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.