Kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imefanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanda miti 5000 kwenye maeneo mbalimbali ya watu binafsi na Taasisi.
Katika kuhitimisha zoezi la kupanda miti jana terehe 7,Disemba 2022 Viongozi wa Wilaya na watumishi wa Halmashauri wameshiriki upandaji wamiche ya miti 500 katika eneo la Hospitali ya Wilaya.
Aidha Halmashauri inaendelea na upandàji wa miti katika maeneo mbalimbali huku elimu ikiendelea kutolewa kwa waananchi juu ya umuhimu wa kutunza mazingira ili kuepukana na athari za mabadiriko ya tabia ya nchi.
Akiongea na watumishi walioshiriki upandaji wa miti katika eneo la Hospitali Ndugu Nyakia Ally Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba amewaasa viongozi wa Hospitali kuhakikisha miti iliyopandwa inatunzwa ili ikue yote, vilevile amewataka Wananchi wote kupanda miti kwenye maeneo yao ili kuendelea kutunza mazingira ya Wilaya hiyo
“ hii miti iliyopandwa itunzwe, tunatarajia kuona baada ya miaka michache hapa pakiwa na mandhari ya kuvutia na kupendeza, lakini mkapande miti kwenye maeneo yenu, pandeni kwa wingi miti ya matunda” amesema Nyakia
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba inaendelea kutekeleza maelekezo ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philipo Mpango ya kupanda miti mingi ili kupambana na mabadiriko ya tabia ya nchi. Katika kutekeleza hilo Halmashauri inatarajia kugawa miche ya matunda kwa wananchi na taasisi.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.