Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba Mh. Peter Lucas Ngassa ameongoza sherehe ya kusaini mikataba ya miradi ya matengenezo ya barabara pamoja na ukarabati wa miundombinu katika hospitali ya Ngudu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 itakayogharimu kiasi cha Tsh.807,933,260 Tarehe 28/02/2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bibi Pendo Anangisye Malabeja amesema Wakandarasi wazingatie kanuni, sheria, taratibu na uadilifu mkubwa wakati wa kutekeleza shughuli zao pia kutojihusisha na vitendo vya rushwa. Maana kufanya hivyo miradi haitatekelezwa kwa viwango tunavyotarajia hivyo kusababisha kukosekana kwa thamani halisi ya fedha katika mradi (Value for Money). Pia amesisitza kuwa Kwimba lazima iwe mfano wa kuigwa kwa kutojihusisha na maswala ya utoaji na upokeaji wa rushwa (Free zone corruption)
Pamoja na hayo Mh. Peter Lucas Ngassa amesisitiza suala la ubora na ufanisi wa kazi.
“Hakikisheni kazi mtakazozifanya zikidhi malengo na matarajio ya serikali na wananchi ili kuleta tija kulingana na pesa iliyolipwa kwa kufanya hivyo mtakuwa mnajenga picha nzuri ya makampuni yenu na mtakuwa msaada kwa serikali yetu inayoimiza uchapakazi wenye viwango”
Vivyo hivyo amesisitiza wakandarasi washirikiane na kujenga mahusiano mazuri na viongozi mbalimbali ngazi ya vijiji na kata ambapo utekelezaji wa miradi hiyo unafanyika ili kuijengea jamii umiliki wa miradi hiyo.
Pia amewaomba wakandarasi hao wamalize kazi zao kwa muda waliopewa kwenye mkataba na malipo yatafanyika baada ya wakaguzi kujiridhisha na kazi na yatafanyika haraka iwezekanavyo.
Wakandarasi waliohusika katika kikao hicho cha kusaini mikataba ni;
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.