Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewataka wazazi wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika Shule za Sekondari Wilayani Kwimba kuwaleta wote kwani Shule zote ziko tayari kuwapokea wanafunzi wote.
Ameyasema hayo leo Agosti 18,2023 wakati akikagua mwenendo wa kuripoti kwa wanafunzi hao katika Shule ya Sekondari Mwamashimba " miundombinu yetu Iko vizuri, Mheshimiwa Rais ametuongezea madarasa nane, mabweni manne na vyoo katika Shule hii na Shule nyingine zote za Kwimba miundombinu imeboreshwa kwahiyo wanafunzi wote waje kusoma na niwahakikishie kuwa Kwimba ni mahali salama, mazingira ya ujifunzaji yako vizuri sana" amesema Ludigija
Aidha Mkuu huyo amewataka wanafunzi wote kuhakikisha wanazingatia masomo yao na kusoma kwa bidii Ili kuongeza ufaulu " mmeona wenzenu waliomaliza kidato cha sita wametufurahisha sana wamefanya vizuri kwenye matokeo yao sasa tunataka nyie mfanye vizuri zaidi ya hao walioondoka " Ludigija
Mkuu wa Shule ya Mwamashimba Mwalimu Ngole Mwanzalima amesema mpaka leo asubuhi wamesharipoti wanafunzi 120 kati ya 400 waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano katika Shule hiyo
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.