Katika kuadhimisha siku ya Uhuru Tanzania bara, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imefanya matukio matatu tofauti leo tarehe 9,Disemba 2022. Matukio hayo ni kufanya mazoezi kwaajili ya kuimarisha Afya za Wananchi ambapo wananchi wamejumuika kwa pamoja kukimbia mchakamchaka kutoka eneo la Uwanja wa Kwideko hadi Ujenzi kisha wakarudi stendi ya zamani.
Baada ya mazoezi hayo wananchi wameadhimisha siku ya Uhuru kwa kufanya usafi katika maeneo ya stendi ya zamani na maeneo ya sokoni. Ambapo wananchi wameshirikiana na watumishi wa umma kufanya usafi katika maeneo hayo.
Katika kujikumbusha hali ilivyokuwa kabla ya uhuru na baada ya Uhuru, umefanyika mdahalo mkubwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ambapo mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa maji, umeme, huduma za Afya, Elimu, utunzaji wa mazingira, uchumi na Usalama wa raia na mali zao.
Akihitimisha Mdahalo huo ndugu Nyakia Ally Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba ameeleza maendeleo tuliyofikia baada ya kupata uhuru
“ tumepiga hatua kubwa sana ya maendeleo baada ya kupata uhuru maana sasa hivi umeme umeenea sehemu nyingi, maji yanapatikana katika maeneo mengi, Elimu inatolewa bila ubaguzi ukilinganisha na kabla ya uhuru, huduma za Afya zinapatikana kuanzia ngazi ya vijiji kwa hiyo tunapaswa kuishukuru Serikali kwani imefanya mambo makubwa baada ya kupata Uhuru”
Katika mdahalo huo wameshiriki wazee ambao baadhi yao walishiriki harakati za kupata uhuru nao wameelezea hali ilivyokuwa kabla ya kupata Uhuru.
” Hali haikuwa nzuri kulikuwa na ubaguzi mkubwa hasa ubaguzi wa rangi mfano siku moja alipita mtoto wa mzungu( mkoloni) akawaamurisha askari watukamate tena anasema kamata hao nyani weusi” amesema mzee Ngobese
Tanganyika ilipata Uhuru tarehe 9,Disemba 1961 chini ya uongozi wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.