Mkoa wa Mwanza umeadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kupanda miti na kuzindua mradi wa maji.Akiongoza sherehe hizo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Ally Kighoma Malima amewataka Wananchi wote kuuenzi na kuutunza Muungano kwani ndio ulioifikisha Tanzania hapa ilipo.
Maadhimisho hayo kimkoa yamefanyika Wilayani Kwimba ambapo shughuli za kupanda miti katika eneo la chuo cha VETA imefanyika na wananchi wametakiwa kuitunza miti hiyo Ili kutunza mazingira na vyanzo vya maji
"hili jambo ni lazima tulifanye tena ni kwa lazima siyo hiari hii nchi ni yetu na kupanda miti nisehemu ya kuinusuru Tanzania na majanga kwahiyo Mwanza tunatakiwa tupande miti millioni 23, katika hili lazima tuwe mfano na siyo kupanda tu ila nikupanda na kutunza" amesema Malima
Mkuu huyo amewataka Wananchi kuendelea kuuenzi Muungano kwa kuhakikisha usalama unaimarika "nchi hii imekuwa ya mfano wa kuigwa kuhusu Muungano maana wengine walijaribu lakini hawakuweza sisi leo miaka 59 tuuenzi Muungano kwa kufanya mambo yanayoleta faida kwa Taifa" Malima
Mheshimiwa Malima amekemea tabia ya baadhi ya wafugaji wanaoharibu miti iliyopandwa makusudi " tunataka tutumie siku ya leo kuelimisha watu umujimu wa kupanda miti, mifugo itakayokamatwa inachungwa kwenye miti faini yake huyo mwenye ng'ombe auze mifugo anunue miti arudishie iliyoliwa yote, lazima watu wajue kuwa kuna eneo la misitu, eneo la kilimo na eneo la kuchungia, wanaofanya uhalibifu wa makusudi msiwaache" Malima
Naye Bakar Mohamed kamanda wa uhifadhi wa misitu Kanda ya ziwa amewashauri Wananchi kuachana na tabia ya kukata miti ovyo,na kulinda miti inayopandwa Ili ikue na isaidie kuleta hewa safi na mazingira bora
Katika maadhimisho hayo mradi wa maji wa millioni 998 umezinduliwa katika Kijiji cha Malenve ambapo tangi la ujazo wa Lita 250,000 limejengwa Kijiji cha ghatuli na vituo vya maji sita vimejengwa, maji yameshawafikia wananchi. Kukamilika kwa mradi huo kumewawezesha Wananchi kutotembea umbali mrefu kufuata maji.
Aidha Mkuu wa Mkoa ametumia maadhimisho hayo kuwashauri wananchi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata chanjo Ili kuwakinga na magonjwa yanayoweza kuzuilika.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.