Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imeadhimiaha kilele cha siku ya mazingira Duniani Juni 5 kwa kupanda miti katika Shule ya Sekondari Bujiku Sakila.
Mkuu wa kitengo cha Maliasili naMazingira Ndugu Deogratias Makungu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji amesema jamla ya miti 874,079 imepandwa maeneo mbalimbali ya Kwimba na katika kuhitimisha zoezi hilo miti 300 imepandwa katika Shule ya Sekondari Bujiku Sakila
" tunapanda miti kukabiliana na mabadiriko ya tabia ya nchi ambayo kwa sasa yamekuwa na madhara makubwa sana" amesema Makungu
Akiwasilisha elimu ya utunzaji mazingira kwa wanafunzi Ndugu Aliko Ndile Afisa Misitu amewaelekeza namna ya kupanda miti na kuitunza, Afisa huyo amewasisitiza wanafunzi kuitunza miti hiyo ili kutunza mazingira na kuepuka madhara yanayosababishwa na uharibifu wa mazingira.
Wanafunzi walioshiriki kupanda miti wameahidi kuitunza na kuilinda na mifugo inayoweza kuharibu " tumepanda hii miti na tumekabidhiwa kila mwanafunzi atatunza mti wake mpaka atakapomaliza kidato cha nne "amesema Gloria Alex
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.