Kwimba yafanya bonanza la kuhamasisha Wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarebe 27 Novemba, 2024.
Bonanza hilo limefanyika leo Septemba 28,2024 kwenye uwanja wa Kwideco ambapo limeongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba Ndugu Mohamed na Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Kwimba Dkt Amon Mkoga ambao wametoa elimu kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Akiongea na makundi mbalimbali yaliyoshiriki bonanza hilo Katibu Tawala amesema " ni muhimu kwa kila Mwananchi mwenye sifa ya kushiriki uchaguzi ajitokeze kushiriki ili tukachague viongozi wanaofaa kutuongoza.
Aidha msimamizi wa Uchaguzi Dkt Mkoga ametumia wasaa huo kuwahamasisha wananchi wote kujitokeza kwenye uandikishaji wa daftari la wapiga kura ambao utaanza tarehe 11-20 Oktoba 2024, pia amewahamasisha wote kujitokeza siku ya uchaguzi kupiga kura kuwachagua viongozi watakaohamasisha maendeleo ya vijiji na vitongoji vyao.
Awali akiongea na waandishi Afisa Uchaguzi wa Halmashauri Ndug. Reginald Clavery amesema Wananchi wanapaswa kutambua kuwa Uchaguzi wa Serikali za mitaa hauna uboreshaji wa daftari ila ni kujiandikisha upya hivyo kila mwananchi atakaye jiandikisha tarehe 11 hadi 20 ndiye atakayeweza kupiga kura.
Afisa huyo amesisitiza kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unalenga kuwachagua wenyeviti wa vijiji,vitongoji na wajumbe wa Serikali ya kijiji na wajumbe wanawake.
Wananchi walioshiriki bonanza hilo wameeleza jinsi walivyo tayari kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa
" mimi niko tayari kujiandikisha na kupiga kura lazima nikawachague viongozi ninaowataka" amesema Mayunga Peter
Bonanza hilo lilisheheni michezo mbalimbali( kuvuta kamba,kukimbia kwenye gunia na michezo mingine) ambapi washindi wa michezo hiyo wametunukiwa zawadi
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.