Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba katika kuhakikisha zoezi la sensa lifanyika kama ilivyokusudiwa leo tarehe 21/08/2022 wamefanya tamasha kubwa la kuhamasisha wakazi wa wilaya ya kwimba kushiriki katika zoezi la sensa litakalofanyika tarehe 23/08/2022 tamasha hilo limefanyika katika viwanja vya kwideko vilivyopo ngudu mjini.
Tamasha hilo limesindikizwa na burudani mbali mbali kama vile mpira wa miguu, riadha kwa wazee wa umri wa miaka 50 na kueandelea na wasanii wa ngoma za asili wakitumbuiza katika tamasha hilo huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya Mhe: Johari Samizi.
Aidha Mkuu wa Wilaya Mhe Johari Samizi amewaasa wakazi wa vitongoji na vijiji vilivyopo katika Wilaya ya Kwimba kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa kwani litasaidia kujua idadi ya watu na makazi kitu kitakachosaidia Serikali kutoa huduma sahihi za kijamii kwa watu sahihi na kwa wakati sahihi na kwa ubora kitu kitakachopelekea chachu ya maendeleo ya kila mmoja na taifa kwa ujumla. Huku kauli mbiu yake ikiwa ni “Tujiandae kuhesabiwa kwa maendeleo ya Taifa letu”
Aidha viongozi mbalimbali wameshiriki katika tamasha hilo na kutoa elimu na semina kwa watu mbali mbali waliofika katika tamasha hilo na kuwafudisha faida za sensa, pia wametoa hamasa kubwa kwa wakazi mbali mbali na kuwaasa wananchi kushiriki kikamilifu na kwa uaminifu na kutoa taarifa zilizo sahihi siku ya sensa.
Aidha wakazi wa Wilaya ya Kwimba wameahidi makubwa katika zoezi la sensa kwani wanasema wapo tayari kuhesabiwa na watashiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kuhuhakikisha wanapata maendeleo kwa wakati sahihi katika taifa lao kwa ujumla.
" tunashukuru tamasha hili limetukumbusha umuhimu wa Sensa na tumejua umuhimu wa kuhesabiwa sasa tutakuwa mabalozi kwa wengine, tutahamasishana ili kila mtu awe tayari kuhesabiwa" amesema Makoye Jumanne
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.