Wakati leo (07/04/2021) ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Aman Karume,Watanzania wamekumbushwa kuendelea kuliombea Taifa,ili kumuwezesha Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake ya kuwaletea maendeleo Wananchi.
Haya yamejitokeza katika Ibada maalumu iliyoandaliwa na viongozi wa Wilaya ya Kwimba kwaajili ya kuliombea Taifa baada ya kuhitimisha kilele cha siku 21 za maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt.John Pombe Magufuli kilichotokea tarehe 17/03/2021.
Ibada hii iliyosheheni nyimbo mbalimbali kutoka kwa wasanii wa nyimbo za injili wameliombea Taifa kuendelea kuwa na amani, umoja na mshikamano baada ya kuondokewa na Hayati Dkt.John Pombe Magufuli, aidha wamemuombea Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kuwaongoza vyema Watanzania.
Wakiongea katika Ibada hiyo viongozi wa dini za Kikristo na kiislam wamesema wananchi wote wanapaswa kuendelea kumuombea Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kuwaongoza wananchi chini ya Uongozi wa Mungu ili malengo ya wananchi ya kupata maendeleo yatimie kama wanavyotarajia.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi Ngaga amewashukuru wananchi wote wa Kwimba kwa kujitokeza kuliombea Taifa pia amesisitiza kufanya kazi kwa bidii kwani maombolezo yamekwisha sasa ni kuchapa kazi tu.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bib. Pendo Malabeja amewaasa wananchi na watumishi wote kuendelea kuchapa kazi baada ya maombolezo ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwani maendeleo ya Wilaya ya Kwimba yatatokana na ushirikiano wa watumishi na wananchi wote.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.