Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imekuwa miongoni mwa Halmashauri sita zilizopatiwa ushindi katika maonyesho ya nanenane Kanda ya ziwa Magharibi yanayojuisha Mikoa mitatu yaani Mwanza,Geita na Kagera yaliyofanyika Nyamhongolo Jijini Mwanza.
Akihitimisha maonesho hayo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa CPA Amos Makala amewapongeza watu wote walioshiriki maonesho hayo kisha amewataka vijana wote kujikita kwenye kilimo kwani ni ajira ya kudumu
" ukizingatia kauli mbiu ya mwaka huu inayosema vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula, Kuna haja ya kuonyesha kuwa kilimo ni ajira kwa vijana Ili vijana waachane na mambo ya kutaka mafanikio ya haraka" Makala
Mkuu huyo ametoa Rai kwa Maafisa ugani kuhakikisha wanaendelea kuwatembelea wakulima na kuwaelimisha Ili kilimo wanachokifanya kiwe na tija.
Aidha Mkuu huyo amewashauri viongozi wa Mikoa yote mitatu yaani Mwanza,Kagera na Geita kwenda kuwa mabalozi kwa kuanzisha mashamba darasa yatakayotumika kuwahamasisha watu wengine hasa vijana kuona umuhimu wa kilimo.
Mheshimiwa Makala ameitumia nafasi hiyo kuwashauri Wananchi wote kujifunza kilimo kutoka kwa wataalamu wa kilimo siyo kudanganyika na kilimo cha mitandaoni ambapo watu wanashawishiwa kufanya kilimo ambacho hakina uhalisia kitu kinachopelekea kukata tamaa pale matokeo yanapokuwa tofauti na walichojifunza mitandaoni.
Wakulima walioshiriki maonesho hayo wameahidi kwenda kufanyia kazi yote waliyojifunza Ili waweze kuboresha uzalishaji katika mazao wanayolima.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.