Hitimisho la maonyesho ya nanenane Kanda ziwa magharibi ambayo yamefanyikia Mkoa wa Mwanza yakiwa yamejumuisha mikoa mitatu yamefungwa na Jenerali Marco Kaguti RC Kagera ambapo katika hafla hiyo halmashauri zote za mikoa ya Mwanza,Kagera na Geita zimeshindanishwa katika maonyesho yao ya kilimo na ufugaji hapo Kwimba imekuwa mshindi wa tatu hivyo kupatiwa zawadi ya cheti na kombe ambalo limepokelewa na katibu tawala wa Wilaya ya Kwimba Ndug. Ally Nyakiha.
Wakulima binafi nao hawakubaki nyuma mkulima Cosmas Sahani kutoka Kwimba amekuwa mshindi wa tatu Kati ya wakulima wote walioshiriki maonyesho na hivyo kuzawadiwa cheti na fedha.
Katika sherehe hizo mgeni rasmi Jenerali Marco amewapongeza waandaaji wa maonyesho hayo na amewapongeza wadau wote na wananchi waliojitokeza katika maonyesho ya nanenane,aidha Jenerali Marco anatamani siku moja Mkoa wa Mwanza uandae Maonyesho ya kitaifa.
Katika sherehe hiyo Mhe.Kaguta amewashauri wananchi kuifanyia kazi elimu waliyoipata katika viwanja hivyo vya nanenane Nyamongolo kuongeza teknolojia katika shughuli za kilimo na ufugaji Kama wakulima walivyoonyesha.
Aidha Jenerali Marco amewataka wakulima kujikita katika kilimo chenye tija yaani kilimo biashara ili thamani ya kilimo iongezeke,pia amependekeza wakulima waongeze kasi kulima hasa chakula kwani soko nilakutosha kutokana mikoa hii ya Kanda ya ziwa kuzungukwa na Nchi nyingine ambazo zinaweza kuuziwa mazao yanayozalishwa hapa nchini.
Akihitimisha hotuba yake amewataka wananchi kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta mbalimbali hasa ya miundombinu kwani ndiyo itakayotumika kusafirisha mazao yetu, pia amesisitiza kauli mbiu ya nanenane 2020 inayosema kwa maendeleo ya kilimo, mifugo na uvuvi chagua viongozi bora 2020.
Hivyo ameshauri wananchi kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo katika Taifa letu.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.