Timu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imeibuka mshindi wa tatu mpira wa mikono ( handball) katika mashindano ya SHIMISEMITA yaliyofanyika Mkoani Dodoma ambapo katika mashindano hayo Halmashauri 70 zimeshiriki. SHIMISEMITA ni mashindano ya michezo Kwa watumishi wa Serikali za Mitaa.
Akipokea kombe kutoka kwa wachezaji hao Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewapongeza watumishi wote walioshiriki michezo hiyo na amewataka kuongeza bidii katika kufanya mazoezi Ili awamu ijayo Kwimba iwe mshindi wa kwanza
" tunataka michezo ifanye vizuri zaidi ili watu waifahamu Kwimba kupitia michezo na mambo mengine mazuri tunayofanya" Ludigija
Kombe hilo limekabidhiwa leo Novemba 9,2023 katika mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/24.
Katika Baraza hilo yamejadiliwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha Waheshimiwa Madiwani kusimamia utekelezaji wa miradi katika maeneo yao
" Madiwani simamieni miradi yote inayotekelezwa katika Kata zenu na ukibaini mradi hauendi sawa toa taarifa" Ludigija
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga akiwasilisha taarifa ya robo amesema Halmashauri inaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo katika robo hii zaidi ya milioni 800 zimepokelewa kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.