Wilaya ya Kwimba yapata tuzo baada ya kuongoza kimkoa katika matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2021.Tuzo hizo ambazo zilitolewa katika kikao cha wadau wa Elimu kilichofanyika siku ya ijumaa ya tarehe 22/4/2022, zilitolewa na katibu tawala mkoa wa Mwanza Ndugu Ngusa Samike katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Mwanza
Kwimba imejipatia tuzo mbili kutoka katika shule mbili ambazo zimeongoza kimkoa ya kwanza ikiwa shule ya sekondari sumve na ya pili ikiwa Shule ya sekondari Mwamashimba, tuzo hizo zimepokelewa na Mkuu wa Wilaya Mhe Johari Mussa Samizi.
Katika Kikao hicho ambacho kililenga kueleza na kutatua changamoto zinazoikumbuka sekta ya Elimu Mkoa wa Mwanza,kilianza kwa kueleza changamoto,ambapo changamoto kubwa ikielezwa ,uhaba wa walimu hasa wa masomo ya sayansi, upungufu wa mabweni kwa baadhi ya Shule, na changamoto nyingine ambapo katibu tawala amewaeleza wadau hao wa Elimu kuwa
"serikali itatatua changamoto hizo na pia nipende kuwaomba tuendelee kufundisha kwa kuzingatia taratibu za Wizara ya Elimu ili wanafunzi wetu wapate Elimu iliyobora na kuongeza ufaulu zaidi ya huu tulioupata 2021"
Naye Afisa Elimu wilaya ya kwimba Mwalimu Emmanuel Katemi anaeleza mipango na mikakati waliyopanga katika kuhakikisha ufaulu unaongezeka zaidi
"kwanza ni kuhakikisha walimu wanatimiza wajibu wao, pia wanafunzi kujifunza kwa vitendo, lakini pia Walimu kukamilisha mada kwa wakati, swala lingine ni kudhibiti vitendo vya utoro na kingine ni kuweka vikao vya idara vya masomo ili viimalishe na kujenga uwezo wa somo husika"
Aidha Afisa Elimu Taaluma Wilaya ya Kwimba Mwalimu Silvia Ntigiri anaeleza malengo yao katika kuongeza ufaulu wilayani hapo
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.