Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imepongezwa kwa kupata hati safi, pongezi hizo zimetolewa na viongozi walioshiriki Baraza la hoja lililofanyika Leo Juni 25,2024 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Akiongea katika baraza hilo Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Elikana Balandya ameipongeza Halmashauri kwa kuweza kupunguza hoja kutoka hoja 70 hadi kubaki na hoja 11, pia amewataka Waheshimiwa madiwani kushirikiana na watumishi wa Halmashauri katika kusimamia utekelezaji wa miradi ili kuondoa hoja za miradi kutokukamilika
' ni vizuri Madiwani mkishirikiana na watumishi kusimamia utekelezaji wa miradi ili ikamilike na muondokane na hoja za miradi ambayo haijakamilika'
Aidha Balandya amezitaka taasisi za umeme na maji kushirikiana na Halmashauri ili kufikisha huduma hizo kwenye vituo ya Afya ambavyo bado havijaanza kutoa huduma kwa wananchi kutokana na kukosekana kwa maji na umeme.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kwimba ameipongeza Halmashauri kwa kupunguza hoja za miradi ambayo haijakamilika na kupata hati safi.
Akiwasilisha taarifa ya mkaguzi wa hesabu za serikali ndugu Mustapha amesema kwa hesabu za mwaka 2022/23 Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ilipata hati ya kuridhisha na kwa miaka mitatu mfululizo kwimba imepata hati safi.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Happiness Msanga amesema Halmashauri inaendelea kujibu hoja ambapo mwaka 2021 Halmashauri ilikuwa na hoja 70 zilijibiwa hoja 69 ikabaki moja, mwaka 2021/22 zilikuwa hoja 62 zilifutwa 59 zikabaki tatu na mwaka 2022/23 hoja zilikuwa 28 zilifutwa 21 zikabaki saba na mpaka sasa Halmashauri ina hoja 11 ambazo ziko hatua mbalimbali za utekel
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.