Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba inafanya maonyesho ya nanenane ambayo yanafanyika kimkoa eneo la Nyamongolo Mwanza,Halmashauri imejikita kuonyesha na kutoa elimu ya shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali yanayopatikana Kwimba ambayo ni Pamba,mpunga,Mahindi,mtama,uwele,Alizeti,dengu,choroko,Mhogo,viazi lishe,matunda aina ya tango na tikiti maji na kilimo cha mbogamboga.Katika maonyesho hayo Idara ya mifugo na uvuvi wanayo mifugo ambayo ni Mbuzi wakubwa sana,kuku,sungura na wanatoa elimu kuhusu ufugaji wa samaki pamoja kilimo cha malisho ya mifugo.
Aidha katika maonyesho hayo Wilaya ya Kwimba inayo mabanda ya wajasiliamali wadogowadogo ambao wanavitu mbalimbali walivyovitengeneza na kuvizalisha,ambavyo ni mafuta ya alizeti,maboga makubwa,unga wa mhogo,sabuni,mchele,asali na vitu vingine.
Wananchi wote wanakaribishwa katika maonyesho hayo ili kujipatia vitu mbalimbali na kupata elimu ya kilimo bora cha mazao mbalimbali na elimu ya ufugaji wa mifugo aina zote.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.