Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imekabidhi millioni 265 Kwa vikundi 21 vya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.Umekuwa utaratibu wa Halmashauri kutoa asilimia kumi ya mapato ya ndani Kwa vikundi vya ujasiliamari kama mikopo isiyo na riba.
Akiongea Kabla ya kukabidhi hundi ya millioni 265,206,226.84 Kaimu Mkurugenzi Ndugu Samweli Joshua Mgoli amewataka watu wote waliokopeshwa mikopo hiyo kwenda kufanya kazi ilivyokusudiwa, vilevile amewataka kuhakikisha wanarejesha fedha hizo Kwa wakati Ili ziweze kutumika kukopesha vikundi vingine
"hii ni fedha ambayo Ina mashariti kwahiyo ukikopa lazima urejeshe, mambo ya kukamatana siyo mazuri sana rejesheni Kwa hiari yenu msisubiri kukamatwa na kupelekwa mahakamani,ukweli ni kwamba dawa ya deni ni kulipa kwahiyo jitahidini kurejesha Kwa wakati" amesema Mgoli
Naye Afisa maendeleo ya jamii (W) Bi. Rosalia Magoti akiwasilisha taarifa ya mikopo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kuanzia mwaka 2016 hadi Sasa 2023 imeshatoa bilioni 1.6 Kwa vikundi 285. Amesisitiza kuwa fedha inayokabidhiwa Leo inatolewankwa Kwa vikundi 21.
Aidha Mkuu wa Kitengo cha Sheria Ndugu Denis Kabogo amewashauri kurejesha fedha Kwa wakati na kwenda kutumia fedha hizo Kwa malengo yaliyokusudiwa, amesisitiza kuwa Sheria zinazosimamia utoaji wa mikopo zitazingatiwa kwa wote watakaokiuka taratibu za mikopo hiyo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.