KWIMBA YAWAENZI MASHUJAA KWA KUSHIRIKI UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Posted on: July 27th, 2024
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imeadhimisha siku ya mashujaa kwa kushiriki shuguli mbalimbali za usafi ikiwa ni pamoja na kufyeka, kupanda miti na kufagia maeneo ya Kituo cha Afya Ngudu.
Akiongea na watumishi walioshiriki usafi Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba Ndugu James Chuwa amewataka wananchi kuwa na tabia ya kuwakumbuka mashujaa wa Taifa la Tanzania na kuwaenzi kwa kufanya kazi kwa uzalendo.
Awali Kaimu Mkurugenzi Ndug. Denis Kabogo amewataka watumishi na wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya usafi maeneo ya taasisi ili kukinga milipuko ya magonjwa yanayoweza kusababishwa na uchafu
"tujenge tamaduni za kushiriki shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira, pia kufanya usafi maeneo ya Hospitali kunasaidia kupunguza magonjwa yanayoweza kusababishwa na uchafu"
Aidha jumamos ya leo imetumika kupanda miti na kufanya usafi ikiwa ni utaratibu wa kufanya usafi kila jumamos ya mwisho wa mwezi