Halmashauri ya wilaya ya Kwimba imezindua rasmi jukwaa la uwezeshaji Wanawake kiuchumi siku ya tarehe 9\5\2017, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya kwimba. Uanzishwaji wa jukwaa hili ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hasani likiwa na lengo la kujadili fursa, changamoto na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika biashara na shughuli zingine za kiuchumi.
Kaim Afisa Elimu Sekondari Bw Boniventure Ng’andilo ambaye alikuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba katika hafla hiyo alitoa wito kwa wanawake wa Wilaya ya Kwimba kuzitumia vizuri fursa mbalimbali zinazowazunguka katika maeneo wanamoishi ili kujikwamua na hali duni ya maisha kwani anatambua kuwa mwanamke anaweza, jamii iwape nafasi ili waweze kuleta mabadiliko katika masuala mazima ya maendeleo.
Aidha, Bw Boniventure Ng’andilo amevihasa vikundi vinavyopata mikopo vitumie vizuri mikopo inayopatikana na kurejesha kwa wakati ili vikundi vingine viweze kukopeshwa.
Akitoa maoni yake katika hafla hiyo, Bibi Christina Bunini ambaye pia ni Kaimu Afisa utumishi
wa Wilaya ya Kwimba amewataka wajasiliamali wenzake kuwa na lugha nzuri katika maeneo yao ya biashara kwani ni mbinu mojawapo ya kuvutia wateja kwenye biashara.
Naye Bi Happy Kaali, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Ngudu aliongeza kwa kueleza kwamba muda ni zawadi kutoka kwa Mungu hivyo ni vyem ukatumika vizuri katika biashara kwani kwa kufanya hivyo malengo yataweza kufikiwa kwa asilimia nyingi zaidi.
Kwa upande wake, Bi Flaviana Moro ambaye ni Mratibu wa uwezeshaji kiuchumi ametoa pongezi za dhati kwa Taasisi zisizo za Kiserikali, asasi za kidini, wadau wa maendeleo, vikundi pamoja na wanawake wajasiliamali kwa kukubali wito wa kuunda jukwaa la Wanawake na amewatakia utekelezaji mwema wa majukumu ya jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi.
Uzinduzi wa jukwaa hilo wilayani kwimba umekwenda sambamba na mafunzo ya ujasiliamali kwa ajili ya kuwainua wanawake Kiuchumi.
Atupakisye M. Mwakalembusya
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.