Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza kamati ya maandalizi ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima (Nane nane) 2024 kwa maandalizi ambayo yamefanyika katika viwanja vya Nyamhongolo wilayani Ilemela.
Mhe. Mtanda ametoa pongezi hizo leo Agosti 08, 2024 wakati alipokuwa akihutubia wananchi waliojitokeza katika kilele cha sherehe za Nane nane Kanda ya Ziwa Magharibi (Mwanza, Geita na Kagera), Mhe. Mtanda amesema amefanikiwa kupita katika mabanda mbalimbali ya waoneshaji ameona na kujifunza teknolojia mbalimbali hakika lengo lililokusudiwa limefanikiwa.
"Nimefurahi kuona baadhi ya bidhaa na huduma zinazopatikana katika maonesho haya, nimetembelea makampuni, Taasisi, huduma za kifedha za mikopo ya kilimo, Taaisisi za elimu na zile za utafiti mkusanyo wa wadau wote hawa umechangia hamasa kubwa kwa wananchi wetu wa kanda ya ziwa nawapongeza na kuwahukuru sana". Mhe. Mtanda.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema katika maonesho hayo Wakulima na wananchi kwa ujumla pia wamepata nafasi ya kuona, kujifunza na kubadilishana uzoefu, teknolojia juu ya bidhaa na huduma mbalimbali na hivyo kupanua wigo wa uelewa kuhusu uzalishaji, uongezaji thamani wa mazao pamoja na mtandao wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa.
"Maonesho haya pia yametumika kuonesha mafanikio yaliyofikiwa pamoja na changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ndivyo ambavyo watu wengi wetu tunatarajia kuona mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye sekta hizi za kiuchimi". RC Mtanda.
Akuzungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigella ameipongeza pia kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo huku akisema amekuwa akihudhuria maonesho hayo kwa kipindi cha miaka miwili lakini sherehe za mwaka huu zimefana sana.
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ni miongoni mwa Halmashauri za kanda ya ziwa magharibi zilizoshiriki maonesho hayo huku Kwimba ikiibuka mshindi wa tatu Mkulima bora wa malisho na Mkulima bora wa zao la pamba.
Maonesho na sherehe za Wakulima kwa mwaka 2024 yamefanyika kwa kauli mbiu isemayo "Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.