Watendaji wa Kata wametakiwa kuelimisha Wananchi kuhusu Lishe bora kwa watoto na kuhakikisha siku ya lishe ya Kijiji inafanyika kila baada ya miezi mitatu.
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija wakati wa kikao cha tathimini ya lishe kilichofayika Leo Mei 2,2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa Watendaji wa Kata ni wakurugenzi katika maeneo yao ya kazi hivyo wanatakiwa kusimamia shughuli zote ikiwa ni pamoja na kuifanya agenda ya lishe kuwa agenda ya kudumu katika mikutano yao
" nendeni mkawaelekeze wananchi juu ya umuhimu wa Lishe Kwa kuhakikisha mnaadhimisha siku ya lishe ya Kijiji kila baada ya miezi mitatu tunasiitiza kuwa tunataka tuwe na watu wenye uwezo wa kufikiri na huo uwezo hauwezi kupatikana kama watoto hawapati lishe bora" Ludigija
Mkuu wa Wilaya ameitumia nafasi hiyo kuwataka Watendaji kusimamia kwa weledi utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao ya kazi pia amewataka kusimamia fedha ya Serikali kwa umakini na kuwataka wawaelekeze wataalamu walio katika Kata zao kutumia fedha za miradi kwa malengo yaliyokusudiwa
" jiepusheni na vishawishi vinavyoweza kukusababisha utumie fedha ya Serikali kwa matumizi yako binafsi, epukeni vitu vinavyodhaririaha utu wenu" amesema Ludigija
Nao Watendaji wameahidi kwenda kufanyia kazi maelekezo waliyopewa ikiwa ni pamoja na kusimamia siku ya lishe ya Kijiji Ili kuboresha lishe za watoto.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.