Serikali kupitia mpango wake wa elimu bure imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kuwasaidia watu wazima ambao hawakupata nafasi ya kupata Elimu kwa utaratibu uliowekwa wanapata Elimu hasa kusoma ,kuhesabu na kuaandika kupitia mpango huu wa Elimu ya watu wazima.
Elimu hii ya watu wazima imeonekana kuwasaidia watu wengi kujua kusoma na kuandika haya yamedhihirika katika maadhimisho ya Elimu ya watu wazima ambayo kwa Mkoa wa Mwanza yamefanyika Wilayani Kwimba tarehe 16/10/2020.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Sweda(wakatikati) akimpongeza Mwalimu aliyeendaa darasa linaloongea katika Shule ya Msingi Mwandu Kwimba.
Akiongea na wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo Mgeni rasmi Mhe.Senyi Saimon Ngaga Mkuu wa Wilaya ya Kwimba akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema serikali inajitahidi kufuta ujinga kwa kuhakikisha hata ambao hawakupelekwa Shuleni kusoma wajifunze (KKK) yaani kusoma kuandika na kuhesabu,pia amesema serikali imeanzisha vyuo vingi nchini yaani FDC,VETA na Mpango wa kujiendeleza kwa masomo ya Sekondari QT ili watu wazima wajiendeleze ametolea mfano wa chuo Cha maendeleo ya wananchi Malya kinatoa fani mbalimbali ikiwemo ufundi wa magali,umeme,fundi bomba, ushonaji na fani nyingine nyingi vyote hivyo nikuwasaidia watu wazima kujiendeleza.
Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuliwa na wataalamu wa Elimu kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza walipata nafasi ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kwimba kuona madarasa yanayoongea na vikundi vya mkeja, baadhi ya vikundi wameishukuru Serikali kwa kuanzisha utaratibu huo wa kuwafundiksha kusoma na kuandika kwani wanafurahia mafanikio hayo maana waliweza kusoma risala zao kuonyesha wazi kuwa wameshajua kusoma na kuandika.
Watu wazima wakisoma risala yao kuonyesha wazi kuwa wamenufaika na Mpango wa KKK (kusoma kuandika na kuhesabu)
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.