Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Adam Malima ametoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu za kazi, ameyasema hayo leo Mei 1,2023 wakati wa maadhimisho ya sherehe ya wafanyakazi iliyofanyika kimkoa Wilayani Sengerema.
Mheshimiwa Malima amewaelekeza viongozi mbalimbali kwenda kufanyia kazi changamoto zilizowasilishwa kwenye risala ya wafanyakazi huku akiwaahidi watumishi hao kutatua changamoto zilizo ndani ya uwezo wake na nyingine kuzifikisha mahali sahihi Ili zitatuliwe.
Mkuu huyo amewapongeza watumishi wote walioshiriki maadhimisho hayo na akasisitiza kuendelea kufanya kazi Ili kujenga nchi
"wito wangu kwenu najua watumishi mnafanya kazi nzuri sana lakini nendeni mkaongeze juhudi zaidi katika uwajibikaji Ili tuunge mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuleta maendeleo ya Taifa hili" Malima
Sherehe za wafanyakazi Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 Mei, Mkoa wa Mwanza umeadhimisha sherehe hizo Wilayani Sengerema ambapo watumishi wameshiriki michezo mbalimbali na watumishi hodari wamepongezwa.
Watumishi walioshiriki maadhimisho hayo wameiomba Serikali kutatua changamoto zilizoorodhesha kwenye risala yao huku wakisisitiza kauli mbiu ya sherehe hiyo ifanyiwe kazi.
Kauli mbiu "MISHAHARA BORA NA AJIRA ZA STAHA NI NGUZO KWA MAENDELEO YA WAFANYAKAZI,WAKATI NI SASA"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.