Maadhimisho ya Siku wa wanawake kimkoa yamefanyika Wilayani Kwimba ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima ameitumia siku hii kuwaasa wananchi kutobagua watoto katika kuwapa Elimu
" Wananchi nazani mmeona hao wanawake wote waliopita na mabango wakiandamana wamesomeshwa na wazazi wao hawakubaguliwa Kwa sababu niwanawake kwahiyo niwashauri muwape kipaumbele watoto wa kike kwenye swala la Elimu" Malima
Mheshimiwa Malima amesisitiza malezi bora Kwa watoto, amekemea ukatili wa kijinsia, kimwili na kiuchumi, amesisitiza wazazi hasa wa kike kujenga mahusiano mazuri na watoto Ili kujua changamoto zote zinazowakabili na kuweza kuzitatua.
Mkuu huyo amekabidhi majiko ya gesi na vifaa vya kujifungulia Kwa wanawake wajawazito kutoka Kata za Kwimba, vifaa hivyo vimetolewa na mashirika mbalimbali yenye lengo la kuboresha maisha ya wanawake wjawazito.Pia amekabidhi taulo za kike Kwa wanafunzi wa kike wa Shule za Sekondari.
Katika maadhimisho hayo ameshiriki Waziri wa Ardhi Mhe Angelina Mabula na Naibu Waziri wa Maliasil na Utali ambao wamewapongeza wanawake wote walioshiriki maadhimisho huku wakisisitiza malezi bora Kwa watoto wakike na wakiume Ili kuwaepusha na madhara yanayosababishwa na mmomonyoko wa Maadili.
Aidha viongozi hao wamewataka wanawake wote wanaopewa nafasi ya kuongoza wajiamini na wafanye kazi zao Kwa weledi Ili waunge mkono juhudi za Mheshimiwa Rais za kuwaletea Wananchi maendeleo
"awe kiongozi wa kikundi,awe kiongozi Ofisi za Serikali au taasisi anatakiwa kujiamini Kwa sababu wanawake wamemuweka pale, tulioko maofisini tupo kwaajili ya kutumikia jamii nzima kwahiyo tuangalie watangulizi wetu pamoja na kuangalia Rais wetu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye anatusababishia kutembea kifua mbele maana miradi ya kimkakati inaendelea,miradi ya Afya, amepunguza riba ya Kodi ya Ardhi haya yote yanafanywa na mwanamke shupavu" amesema Angelina Mabula
Siku ya wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi ambapo mwaka huu yamekuwa na kauli mbiu inayosema
"UBUNIFU WA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA, CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.