Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata( ARO Kata) wamepata mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ambapo wamesisitizwa kufanya kazi hiyo kwa weledi huku wakizingatia maadili.
Akifungua mafunzo hayo Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kwimba na Sumve Bi. Happiness Msanga amewataka maafisa hao kwenda kufanya kazi hiyo kwa kuzingatia taratibu zote watakazoelekezwa katika mafunzo hayo.
Amesisitiza kuwa utekelezaji wa kazi hiyo uzingatie maelekezo yote ya uandikishaji na kuzingatia namna bora ya kuwasiliana na utaratibu sahihi wa kutoa taarifa za kazi hiyo.
Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Jimbo wametoa mafunzo namna bora ya kujaza fomu za uboreshaji wa daftari la mpiga kura.
Uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura utaanza tarehe 21 Agost 2024 hadi 27 Agosti 2024 hivyo maafisa hao wametakiwa kwenda kuhamasisha wananchi kujitokeza kuboresha taarifa zao.
Aidha amewataka kwenda kuwatangazia wananchi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la mkazi kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa " wananchi waeleweshwe kuwa kuna daftari la mkazi kwaajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa na daftari la kudumu la mpiga kura kwaajili ya uchaguzi mkuu" amesema Msanga
Maafisa hao wameahidi kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.