Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) imefanya mafunzo kwa Maafisa ugani wa WIlaya ya Kwimba yanayohusu mbinu bora za kilimo cha Korosho,mafunzo hayo yamefanyika tarehe 21/12/2020 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Wataalamu hao wa kilimo kutoka TARI wamesema ili kuzarisha korosho bora Mkulima anapaswa kuzingatia mbinu au kanuni bora za kilimo ikiwemo uchaguzi mzuri wa shamba,matayarisho ya shamba,kutifua ardhi,kulima kwa kuzingatia vipimo sahihi vya umbali kutoka mche mmoja hadi mwingine,aina ya mbegu na mbinu nyingine. Akielezea umuhimu wa kufata kanuni hizo Ndug.Isaya Mwakabega amesema Wakulima wanatakiwa kuelekezwa kanuni hizi ili wanapoanza kulima zao hili wazalishe kwa wingi ili wapate manufaa ya zao la Korosho.
Ndug.Isaya Mwakabega Mtaalamu wa udhibiti wa magonjwa na wadudu waharibifu wa Korosho kutoka TARI Naliendele.(aliyesimama)
Ndug.Bakari Rashidi Kidunda Mratibu wa uhaulishaji wa teknolojia na mahusiano TARI Naliendele Mtwara.(aliyesimama)
Kifaa(Pump) cha kupulizia dawa kwenye miti ya Korosho.
Vifaa vya kupimia shamba wakati wa kupanda miche ya Korosho.
Katika Wilaya ya Kwimba shughuli kuu ya kiuchumi ni kilimo cha Pamba,dengu na choroko hivyo TARI wamefanya mafunzo ya kilimo cha korosho ili zao hilo lilimwe kuona kama litastahimili hali ya hewa ya Kwimba,ikiwa zao hili litastahimili litaongeza mazao ya kiuchumi Wilayani Kwimba.Wakulima wamelipokea zao hili kwa furaha na wanayoshauku kubwa ya kuona matokeo ya zao la korosho.
Kwamujibu wa Wataalam kutoka TARI wanasema Mkulima akizingatia mbinu bora za kilimo cha zao la korosho inawezekana baada ya miaka mitatu Korosho ikaanza kutoa matunda.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.