Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewaelekeza Maafisa Kilimo na Mifugo kuanzisha mashamba darasa ya kilimo yatakayotumika kuwafundishia wakulima kilimo bora na ufugaji.
Ameyasema hayo leo tarehe 7, Novemba 2022 katika kikao cha Maafisa ugani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
“nasisitiza kila mtu akaanzishe shamba darasa ili hayo mashamba yawe mfano hai kwa wakulima siyo mnawafundisha wakulima kilimo bora wakati nyie hata shamba la mfano hamna” amesema Msanga
Aidha Maafisa hao wamesisitizwa kuendelea kutoa elimu ya kilimo na ufugaji kwa Wananchi ili kilimo kiweze kuongeza tija,”msichoke kutoa elimu kwa wakulima, msichoke kuhamasisha kilimo bora” amesema Msanga
Vilevile maafisa ugani wameshauriwa kusimamia vikundi vya kilimo na ufugaji vilivyopewa mikopo na halmashauri kwaajili ya kujishughulisha na kilimo ili viweze kutumia fedha kwa lengo lililokusudiwa.
Naye Afisa Kilimo (W) Mhandisi Magreth Kavalo amewataka maafisa kilimo na mifugo kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi pia amesisitiza uwajibikaji.
Nao maafisa ugani wameeleza changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na uhaba wa maafisa ugani kitu kinachopelekea Afisa mmoja kuhudumia kata zaidi ya moja hali inayopelekea kuhafifisha utekelezaji wa kazi.
“ tunaomba watumishi waongezeke ili iturahisishie kuwafikia wakulima maana mtu mmoja kuhudumia wakulima zaidi ya kata moja ufanisi wa kazi unapungua maana hatuwezi kuwafikia wote” amesema Afisa mifugo Arsen Mwenda
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.