Afisa mradi wa fistula Dkt.Magdalena Dalla kutoka shirika la AMREF akifanya ufuatiliaji wa kazi za uelimishaji kuhusu fistula ya uzazi amewataka mabalozi wa fistula kufanya kazi ya kuwaelimisha watu kuhusu fistula ya uzazi na kuibua wahanga wenye tatizo la fistula ili wapelekwe Hospitali ya Bugando kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.Akiongea na mabalozi hao Dkt.Dalla amesema fistula ni tundu lisilo la kawaida linalotokea Kati ya kibofu cha mkojo au njia ya haja kubwa na uke au vyote kwa pamoja na kusababisha kutokwa na mkojo au haja kubwa bila kujitambua.
Dkt.Dalla amesema mabalozi wa fistula wanapaswa kutoa elimu hiyo ili wahanga wasaidiwe matibabu ambapo wafadhili wametoa fedha ili wahanga wa fistula wafanyiwe upasuaji bure katika Hospitali ya Bugando Mwanza au CCBRT Dar es salaam.
Aidha Dkt Dalla amewashauri mabalozi wanapotoa elimu ya fistula wasisitize kuwa fistula siyo ugonjwa wa kulongwa(kishirikina) Kama wananchi wengi wanavouchukulia bali niugonjwa unaosababishwa na uzazi pingamizi.
Katika zoezi hilo la ufuatiliaji wa kazi za mabalozi wa fistula Bi.Nakaniwa Mshana Afisa ufuatiliaji wa mradi wa fistula kutoka shirika la MAPERECE amewashauri mabalozi kujitolea kuwafikisha wahanga katika vituo vya Afya au Zahanati ili wanapofika hapo wasaidiwe jinsi ya kufika Hospitali ya Bugando kwaajili ya upasuaji. Nakaniwa ameeleza kuwa wahanga wanapofika Bugando kwaajili ya matibabu ya fistula wanahudumiwa bure na nauli wanazotumia wahanga kufika Bugando wanarudishiwa.Nakaniwa amewataka mabalozi wawashauri wahanga kufika Hospitali kwani fistula inatibika.
Wakielezea taarifa za kazi walizozifanya mabalozi wa fistula, wameeleza jinsi walivyoweza kuibua wahanga 23 wa fistula ambapo wahanga 16 niwapya kwa maana kwamba walikuwa hawajapata matibabu yoyote hivyo utaratibu wa kuwafikisha Bugando kwa matibabu umeshafanyika baadhi yao wanaendelea na matibabu na wahanga 7 wamekutwa wakiwa walishatibiwa miaka mingi iliyopitana.
Hii ni kanga wanayopewa wahanga wa fistula wanaokwenda Bugando kufanyiwa matibabu.
Wananchi wote wanapaswa kutowaficha,kutowatenga wala kutowanyanyapaa wagonjwa wa fistula kwani hilo ni tatizo linaloweza kumpata mwanamke yeyote anayepata uzazi pingamizi wakati wa kujifungua.Pia wanawake wanashauliwa kujifungulia katika vituo vya Afya au Hospitali ili kuepuka kupata tatizo la fistula.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.