Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robart Gabriel amepokea madarasa 109 yaliyojengwa kwa bilion 2.18 fedha za UVIKO-19 yakiwa yamekamilika. Akipokea madarasa hayo Mkuu wa Mkoa amewapongeza viongozi wa Wilaya na Halmashauri kwa usimamizi walioufanya mpaka kuhakikisha madarasa hayo yanakamilika. Pia amepongeza wasimamizi kwa kuwezesha mradi kukamilika na chenji kubaki.
Akiongea na Wananchi na watumishi walioshiriki hafla hiyo amewataka Viongozi wote wanaosimamia miradi mbalimbali kuendelea kuwa waadilifu katika utekelezaji wa miradi kwani wezi hawawezi kuheshimika mahali popote pale duniani.
" Hautaheshimika ukila hela za umma, hautaheshimika ukiwa fisadi, hautaheshimika ukiwa mwizi, timiza jukumu lako kwenye nafasi aliyokupa Mungu ndio jukumu letu na tulizike na maisha yetu, wajibu wetu ni kutoa huduma basi"
Katika Hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amewashukuru Wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha katika kufanikisha ujenzi wa madarasa hayo, amesema haikuwa kazi rahisi wasimamizi wote wamejitoa ili kufanikisha kukamilika kwa ujenzi huo.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amemshukuru Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha hizo bilion 2.18 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 109, amesema kupitia madarasa haya wanafunzi wa wataweza kusoma katika mazingira mazuri na rafiki.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.