Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amewataka waheshimiwa Madiwani kuongeza usimamizi wa miradi ya maendeleo
" waheshimiwa madiwani shirikianeni na wataalamu kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yenu, miradi hiyo ikikamilika itawarahisishia kazi nyie kwenye kazi zenu za kisiasa lakini lengo la Serikali litakuwa limekamilika la kuwafikishia huduma wananchi" amesema Ludigija
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka TARURA kuongeza juhudi katika utekelezaji wa miradi ya barabara na madaraja ili kuondoa kero ya kushindwa kipita kwa wakati pindi mvua kubwa inaponyesha mfano daraja la Solwe
Mkuu huyo amewataka watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za utumishi, pia amewasisitiza watumishi wote kujiamini wanapotekeleza majukumu yao.
Akiwasilisha taarifa kaim Mkurugenzi, Ndugu Wiliam Kasuja amesema Halmashauri inaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi aidha katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/25 Halmashauri imepokea watumishi ajira mpya 178 wakiwemo watumishi wa Idara ya Elimu,Afya,utawala na manununi.
Nao waheshimiwa Madiwani wametumia wasaa huo kumuomba Mkuu wa Wilaya kuendelea kuwasisitiza wakala wa barabara kukarabati madaraja na barabara kwa wakati.
Katika mkutano huo ameshiriki Katibu wa CCM Wilaya ya Kwimba Ndug. Agatha Lubuva ambaye amewashauri waheshimiwa Madiwani na watumishi kufanya kazi kwa ushirikiano
"Maendeleo hayawezi kupatikana bila ushirikiano kati ya chama na Serikali kwahiyo watumishi na Madiwani tushirikiani ili tuijenge Kwimba na Taifa kwaujumla"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.