Madiwani wawasirisha taarifa zao za kata katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika tarehe 12/02.2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.Kamati mbalimbali nazo zimetoa taarifa zao ikiwemo kamati ya Elimu,Afya na maji ambapo kamati imeshauri Waalimu wakuu wawe wanabadirishiwa vituo vya kazi ili kuongeza ufanisi na ufaulu katika kazi,pia wamesisitiza wahudumu wa Afya yaani waganga na manesi kuishi karibu na vituo vyao vya kutolea huduma.
Katika kikao hicho madiwani wameiomba Serikali kununua gari la zimamoto ili kurahisisha uokoaji pindi ajali za moto zinapotokea, haya yamejitokeza baada ya taaarifa ya kamati ya uchumi ambayo imesisitiza kila taasisi ya Serikali kuwa na vifaa vya zimamoto na Elimu itolewe kwa wananchi ili wapate uelewa kuhusu majanga ya moto.
Katibu wa kikao hicho ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri Bib.Pendo Malabeja ameshauri madiwani kusaidia kusimamia ukusanyaji wa mapato unaofanywa na watendaji wa kata na vijiji,vilevile amesisitiza kuwa nimakosa kwa kiongozi wa Serikali kutumia pesa ya Serikali isivyostahili 'ni makosa makubwa mtumishi kutumia fedha zile anazozikusanya kama mapato ya Halmashauri' amesema Malabeja.Pia ametoa taarifa kuwa ametoa maelekezo kwa watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha kila shule inakuwa na kalakana ndogo kwa ajili ya ukarabati wa viti,meza na madawati ya wanafunzi.
Aidha katika kikao hicho Katibu Tawala wa Wilaya Ndug.Nyakia Ally amesisitiza madiwani na watendaji kusimamia miradi ya maendeleo inayoendelea na amewashauri madiwani kwenda kuwashirikisha wananchi kuhusu miradi inayoendelea ili wawe na uelewa wa pamoja kuhusu miradi inayotekelezwa katika kata zao,vilevile Katibu Tawala nae amesisitiza suala la kila Shule kuwa na kalakana ndogo kwa ajili ya ukarabati wa viti,meza na madawati ya wanafunzi ili kalakana kubwa ya kutengeneza vit,meza na madawati ibaki Halmashauri.
Katibu Tawala wa Wilaya Ndug.Nyakia Ally
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kwimba Bib.Pendo Malabeja
Mwenyekiti kamati ya Elimu,Afya na maji Mhe.Kapunda
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.