Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango yawapongeza wasimamizi wa miradi inayotekelezwa . Haya yamejitokeza katika ziara ya kamàti hiyo iliyofanyika tarehe 21-22,Aprili 2022 Wilayani Kwimba.
Katika ziara hiyo wajumbe wametembelea mradi wa ujenzi wa Shule mpya za Nkalalo na Kilyaboya zinazotekelezwa kwa milion 940 ambapo katika miradi hiyo madarasa, maabara, jengo la utawala, maktaba, jengo la komputa na matundu ya vyoo yanaendelea kujengwa kwa kuzingatia ubora unaotakiwa. Wajumbe hao baada ya kuona miradi hiyo na hatua iliyofikiwa wamempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri na kamati nzima inayohusika na usimamizi wa majengo hayo huku wakiwataka wasimamizi hao kuongeza kasi zaidi ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati kama ilivyokusudiwa.
Kamati hiyo imekagua ujenzi wa Vituo vya Afya Isunga na Hungumalwa ambapo Hungumalwa walipokea milioni 500 za ujenzi huo huku Isunga wakipokea milion 250.Vituo vyote vinatekelezwa kwa kasi ya kulizisha na kamati hiyo imepongeza juhudi za usimamizi wa miradi hiyo.
Aidha kamati imekagua ukamilishaji wa Zahanati ya Mwankuba milion 50 na Ujenzi wa madarasa sita katika Shule ya Msingi kabale milioni 121 miradi inayotekelezwa kwa fedha za mapato yandani, hapo wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Theleza Lusangija wameipongeza Halmashauri kwa kujenga madarasa ya Shule ili kuokoa maisha ya wanafunzi yaliyokuwa hatarini. kulingana na madarasa waliyokuwa wakitumia kuchakaa kwa kiwango kikubwa.
Ziara hiyo imelenga kuongeza tija katika utekelezaji wa miradi na kuongeza chachu ya ukusanyaji wa mapato kwani kamati hiyo imefika katika mgodi wa Mhalo kuona shughuli nzima ya uchimbaji wa madini inavyofanyika na jinsi Halmashauri inavyokusanya mapato kupitia mgodi huo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.