Wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya Kwimba( DCC) wameshauri wadaiwa sugu wa madeni ya mikopo ya vikundi vinavyokopeshwa na Halmashauri wakamatwe na jeshi la police kama hawataki kilipa fedha hizo kwa hiari.
“ wadaiwa wakamatwe warudishe fedha ili watu wengine wakopeshwe, tena hiki kikosi kazi kilichoanza kuwakamata kiongeze nguvu zaidi na wanapokamata wasibague, watu wote wanaodaiwa wakamatwe walipe, hatuwezi kubembeleza watu kurudisha fedha wakati walisaini mikataba ya kurudisha fedha hizo ndani ya mwaka mmoja” amesema Majoge Diwani Hungumalwa
Haya yamejiri kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ( DCC ) ambacho kimefanyika leo tarehe 15, Disemba 2022 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi ameshauri vikundi vinavyokopeshwa virudishe fedha hizo kwa wakati wasisubiri hadi wakamatwe ndipo warejeshe
“ dawa ya deni ni kulipa, wanaodaiwa walipe fedha wasisubir kukamatwa, lakini kuhusu elimu vikundi vinapewa elimu kabla ya kukopeshwa kwahiyo kutorejesha ni tabia ambayo vikundi vingi wanafikiri fedha ya Serikali haina mtu wa kuifatilia” amesema Samizi
Aidha Mkuu huyo ameshauri Idara ya maendeleo ya jamii ibadirishe utaratibu wa kutoa mikopo kutoka kutoa fedha hadi kutoa vifaa au vitu ili kuepusha tabia ya baadhi ya vikundi vinavyokopeshwa fedha kisha kubadili matumizi ya fedha hizo badara ya kufanya biashara wanagawana fedha kitu kinachopelekea kushindwa kurejesha fedha hizo.
Nao wafugaji wametakiwa kuacha tabia ya kupitisha mifugo barabarani hali inayosababisha uharibifu wa barabara
“ kamateni mifugo yote inayopita barabarani muwatoze faini ya elfu 50 kila ngombe ili iwe fundisho kwa wafugaji wote wasiotaka kufuata sheria na taratibu za Serikali” amesema Samizi
Katika Kikao hicho taarifa za taasis mbalimbali zimewasilishwa zikiwemo taarifa za RUWASA,TANESCO,TARURA,MWAUWASA,VETA, FDC MALYA NA CHUO CHA AFYA NGUDU.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.