Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewataka Waheshimiwa Madiwani na viongozi wote wa vijiji na Kata kuwa Mabalozi kwa wananchi wao kwa kuwahamasisha ujenzi wa vyoo bora na vya kisasa.
Ameyasema hayo kwenye Baraza la Madiwani la robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/23 lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri
"Madiwani na viongozi katika maeneo yenu mkawe mabalozi, mkaonyeshe kwa mfano ujenzi wa vyoo bora, tunataka Wananchi wote wawe na vyoo bora Ili kujiepusha na mripuko wa magonjwa unaoweza kuepukika" Ludigija
Aidha Mkuu huyo amewaelekeza Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha Kila Shule inatoa chakula kwa wanafunzi kwa kuwashirikisha wazazi kuchangia vyakula vya wanafunzi
" kama watoto wanaokuwa nyumbani wanakula mchana kwanini anayekuwa shuleni kile chakula ambacho angekula nyumbani kisipelekwe shuleni? tunataka watoto wote wapate chakula shuleni Ili waweze kusoma vizuri" Ludigija
Akiwasilisha taarifa ya robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/23 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amesema Halmashauri imepokea kiasi cha Bilioni 2.24 kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu Sekondari. Shule mpya mbili zinajengwa Sumve na Bupamwa na madarasa na mabweni yanajengwa katika Shule za Mwamashimba,Talo, Ngudu,Kilyaboya na Manawa,
Baada ya Baraza hilo ulifanyika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Halmashauri ambapo Mhe. Lameck Hole amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.