Waheshimiwa Madiwani wameshauriwa kusimamia ukusanyaji wa mapato katika kata zao ili kufikia malengo yaliyokadiliwa kwa mwaka. Haya yamejiri katika kikao cha baraza la Madiwani wakati wakiwasilisha taarifa za kila kata ambalo limefanyika leo tarehe 5/9/2022 ambapo baadhi ya Kata zimeonekana kutofikia lengo walilokadiliwa kukusanya.
Madiwani hao wameshauri kata zilizoshindwa kufikia malengo wafanye uchunguzi kujua changamoto zinazopelekea kushindwa kufikia lengo lililokusudiwa ili kuzitafutia ufumbuzi, wamesisitiza kuwa kila kata inatakiwa kukusanya mapato ili kuongeza mapato ya Halmashauri na kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha Waheshimiwa Madiwani wameshauri kata zilizokàdiriwa fedha kidogo, Makadirio hayo yaongezwe ili watendaji waongeze juhudi za ukusanyaji wa mapato.Pia wameshauri mashine za kukusanyia mapato ziongezwe kwa watendaji ili kila kijiji kiweze kushiriki ukusanyaji wa mapato.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mhe.Happiness Msanga alipata wasaa wa kuelezea kuwa Halmashauri inatarajia kununua mashine za kukusanyia mapato (POS) zitakazo pelekwa kila kijiji ili ukusanyaji wa mapato ufanyike maeneo yote,pia amesisitiza kuwa ukusanyaji wa mapato usitegemee mazao tu bali vyanzo vyote vitumike kukusanya mapato.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.