Chuo cha maendeleo ya Wananchi ( FDC) Malya kimefanya mahafali ya 48 ambapo wanafunzi 266 wamehitimu kozi mbalimbali ikiwemo ufundi wa magari, ufundi Bomba, ufundi wa umeme, ufundi wa kushona nguo, kozi ya mifugo, ualimu wa watoto wadogo na wanafunzi wanaosoma Elimu Haina mwisho ambao ni wasichana waliokatiza masomo yao kwa sababu mbalimbali wanapata nafasi yakurudia masomo ya Sekondari.
Mgeni rasmi wa Mahafali hiyo ndugu Hassan Nyagani Meneja wa NMB aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya amewashauri wanachuo hao kwenda kutumia vizuri ujuzi walioupata ili ukaongeze tija kwa Taifa
" Taifa la Tanzania linawategemea sana na Elimu ya ufundi mliyopata inahitajika maeneo mengi kwahiyo katumieni ujuzi huu vizuri katika kuitumikia jamii na Serikali " amesema Nyagani
Akiwasilisha taarifa fupi ya chuo hicho Mkuu wa Chuo Frank Igembe ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuleta fedha za vifaa vya mafunzo ambavyo vimesaidia kuboresha ufundishaji kwa vitendo na hiyo imesaidia kuongeza idadi ya wanachuo.
Aidha Chuo hicho bado kina changamoto ya upatikanaji wa maji jambo ambalo linaendelea kutafutiwa ufumbuzi na uongozi wa Chuo kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya.
Wahitimu wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya Chuo hicho " tunaishukuru Serikali kwa kutujengea madarasa mazuri na kukarabati mabweni lakini pia tumeletewa mashine za kujifunzia ambazo zimeturahisishia ujifunzaji maana tunajifunza Kwa vitendo" amesema Fredy Shagembe
Mkuu wa Chuo ameitumia nafasi hiyo kuwakaribisha Wananchi kuendelea kupeleka vijana kupata masomo katika Chuo hicho ambapo ujuzi mbalimbali unatolewa. Chuo cha FDC kinazaidi ya wanachuo 600 wanaosoma kozi mbalimbali, kinapatikana Kata ya Malya Wilayani Kwimba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.