Katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 11, Agosti 2021 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mkurugenzi Mtendaji Bi. Happiness Joachim Msanga amemshukuru Mungu kwa kumuwezesha kuteuliwa ili kuwatumikia watanzania wa Kwimba, kisha amewashukuru Wakuu wa Idara wote kwa mapokezi waliyompatia na upendo wanaomuonyesha.
Katika hotuba yake fupi kwa wakuu wa Idara Bi.Msanga amesisitiza uwajibikaji, upendo, nidhamu na ushirikiano, amesisitiza kuwa bila ushirikiano hakuna jambo litakalo songa mbele hivyo amewaomba viongozi hao kumpatia ushirikiano kwa kipindi chote atakachofanya kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Aidha Ndug. Alexander S. Ndaro aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi kwa muda wa miezi mitano amewashukuru Wakuu wa Idara na Viongozi wote wa Wilaya ya Kwimba kwa ushirikiano waliomuonyesha kipindi chote alichokaimu Ukurugenzi na ameshauri ushirikiano huo undelee kwa Mkurugenzi huyu anayekabidhiwa Halmashauri.
Katika hafla hiyo Ndugu Nyakia Ally Katibu tawala wa Wilaya amemkaribisha Mkurugenzi katika Wilaya ya Kwimba na anaamini maendeleo yataongezeka " naamini wanawake mnaweza" amesema Nyakia Ally, amesisitiza ushirikiano katika kazi zote na usimamizi wa miradi ili Kwimba isonge mbele.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.