Makamu wa Rais Mhe.Dkt Philip Isdor Mpango amemtaka mhandisi wa barabara Tanrods kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Magu-Ngudu - Hungumalwa ambayo imeonekana kuwa ndicho kilio kikuu cha wananchi wa Wilaya ya Kwimba.
Makumu wa Rais ameyasema hayo leo April 11,2023 wakati alipokuwa akisalimiana na Wananchi wa Kata ya Hungumalwa wakati akipita kuelekea Wilaya ya Misungwi.
Aidha Mheshimiwa Mpango amewapongeza Wananchi wa Kwimba Kwa kuendelea kufanya kazi nzuri na kushiriki kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani hapo
'niwapongeze Wananchi wa Wilaya ya Kwimba hongereni kwa kazi nzuri katika kilimo,mifugo mnafanya vizur hata Afya zenu zinasadifu hilo" amesema Mpango
Mheshimiwa Mpango amewataka Wananchi wote kuhakikisha wanasimamia fedha zote zinazoletwa kwaajili ya utekelezaji wa maendeleo zifanye kazi iliyokusudiwa, amewataka viongozi kuhakikisha fedha hiyo haipotei hata shilingi
" viongozi hakikisheni fedha hii haipotei hata shilingi simamieni vizuri nataka kuona Mkoa wa Mwanza haupati taarifa mbaya kutoka Kwa mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa hesabuza Serikali"
vilevile Makamu wa Rais amesisitiza upandaji wa miti Ili kutunza mazingira na kuepukana na madhara yanayosababishwa na uhalibifu wa mazingira.
Nao wahe.Wabunge wa majimbo ya Kwimba na Sumve wamemshukuru Mheshimiwa Rais kwa fedha anazoleta za kutekeleza miradi mbalimbali,pia wametoa kilio chao cha kuomba kujengwa barabara ya lami ya Hungumalwa- Ngudu - Magu na barabara ya Mabuki Ngudu ambapo Mbunge wa Jimbo la Sumve ameanza kuomba na Mbunge wa Jimbo la Kwimba akakazia
" Wilaya yetu haina barabara ya lami ya kuiunganisha na Wilaya nyingine au Wilaya na barabara kuu tunaomba barabara hii, naomba nikuombe barabara ya Msingi kabisa Kwa uchumi wa Kwimba barabara inayotokea Isandula Magu inapita Ngudu mpaka hapa Hungumalwa, barabara hii inaurefu wa kilomita 71 na Iko ukurasa wa 70 wa ilani ya chama cha Mapinduzi, nakuomba sana katika bajeti ya mwaka huu ianze kujengwa Kwa kiwango cha lami" amesema Kasalali Mbunge Jimbo la Sunve
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.