Shirika la Agriteam health Tanzania lenye mradi wa MAMA NA MTOTO limekabidhi jengo moja la Zahanati lenye jumla ya vyumba 11 kwa ajili ya matumizi ya huduma za kiafya na Nyumba moja ya kuishi watumishi wawili(2 in 1).Katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa mradi wa Mama na Mtoto Ndug:Tanya Salewsky ameishukuru Halmashauri kwa ushirikiano wakati wa mradi na amewaomba wananchi wa Izizimba 'A' kuutunza mradi huo ili wanufaike kwa kupunguza au kuondoa kabisa vifo vya Mama,Baba na Mtoto.Aidha Katibu tawala wa Wilaya Ndug:Ally Nyakia amewashukuru watu wa mradi wa Mama na Mtoto kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya na amewataka wananchi waitumie Zahanati hio vizuri hasa wanawake wameshauriwa kujifungua kwenye zahanati siyo nyumbani ili kuepusha vifo vya mama na mtoto.Mkurugenzi wa Halmashauri Ndug: Pendo Malabeja amewashukuru (Agriteam) Mama na Mtoto kwa mradi huu na amewakaribisha Kwimba kuleta miradi mingine yenye manufaa kwa wananchi kama huu wa Zahanati.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.