Viongozi wa dini toka vijiji 119 vya Wilaya ya Kwimba wamefanya maombi ya kuliombea Taifa katika kumbukizi za Baba wa Taifa Mwalimu J K Nyerere,haya yamefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu leo tarehe 14/10/2020.
Viongozi hao wa dini wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Saimon Ngaga wamesisitiza amani,umoja na mshikamano katika kipindi hiki cha kampeni na uchaguzi, vilevile wamesema Mwalimu J K Nyerere alituacha tukiwa wamoja bila udini wala ukabila hivyo umoja huo udumishwe. Aidha wamewashauri wananchi wote kijitokeza siku ya uchaguzi ili wakachague viongozi wanaowapenda kwa manufaa ya Taifa.
Katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya amesisitiza Swala la kumuenzi Baba wa Taifa ili vizazi vijavyo viweze kuutambua mchango wake mkubwa katika Taifa hili.Pia amewashukuru viongozi wa dini kwa ushirikiano wanaouonyesha katika shughuli mbalimbali za Wilaya hii,vilevile amewashauri wananchi wote kujitokeza siku ya uchaguzi kwenda kupiga kura kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya Taifa letu.
Mkuu wa Wilaya akiongea na viongozi wa dini
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kwimba Bib. Pendo Malabeja naye amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa letu ili uchaguzi uishe kwa amani na utulivu na viongozi bora wapatikane pia amewaomba wananchi wote kuendeleza mazuri yote aliyotuachia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kwimba Bib. Pendo Malabeja akiwashukuru viongozi wa dini kwa kuliombea Taifa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.