Mkuu wa Mkoa wa Geita Mheshimiwa Martin Shigela ahitimisha maonyesho ya nanenane kwa kuwashauri watu wote walioshiriki maonyesho hayo kuyatumia kama fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali zitakazopelekea matokeo chanya kwenye Kilimo na mifugo, ameyasema hayo leo tarehe 8,Agosti 2022 katika viwanja vya Nyamhongolo Mwanza ambapo maonyesho ya nanenane kanda ya ziwa magharibi yamefanyikia.
Aidha Mkuu huyo amesema Kauli mbiu ya maonyesho ya nanenane ya mwaka huu inayosema “ Ajenda 10/30 Kilimo ni biashara, shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,mifugo na uvuvi” imelenga kuongeza uzalishaji hivyo ameshauri uzalishaji na biashara ya pamoja kwa mikoa yote mitatu yaani Geita,Mwanza na Kagera uongezeke ili kufikia malengo ya kilimo biashara
“nimetembelea maonyesho nimeona bidhaa za wananchi wanazalisha, wanatumia mbegu bora kazi yetu ni kujifunza na kubadirika tuitumie hii kama fursa ya kuleta mabadiliko, kuongeza uzalishaji,Maonyesho haya yatumike kubadilisha mahusiano, uelewa kwenye kilimo,mifugo na uvivu”amesema Shigela
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Kigoma Malima amewapongeza watu wote walioshiriki maonyesho ya nanenane yakiwemo makampuni, taasisi, Halmashauri na watu binafsi. Amesema maonyesho ya kilimo ni muhimu katika kukuza uchumi ukizingatia kauli mbiu ya mwaka huu.
Mheshimiwa Malima ameshauri changamoto zilizopo kwenye kilimo zitumike kupanga mipango itakayosaidia kanda hii kuinua uchumi kupitia kilimo.
Nanenane ni sikukuu ya wakulima ambayo huazimishwa kila mwaka tarehe 8,Agosti.Kupitia maonyesho hayo wakulima wameonyesha mazao na mifugo mbalimbali ambapo wananchi wameweza kujifunza mbinu za ufugaji na kilimo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.