Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba yaanza kutoa mbolea ya ruzuku kwa Wakulima waliojiandikisha. Zoezi hili limeanza kufanyika jana tarehe 7, Disemba 2022 katika ofisi za Idara ya Kilimo.
Mbolea ya ruzuku inatolewa kwa wakulima waliojisajiri kwenye mfumo wakapata namba zao za siri ambapo wakifika Ofisini hapo wanaonyesha namba zao za siri ambazo zikiingizwa kwenye mfumo zinaonyesha taarifa kamili za mkulima huyo na hivyo kumuwezesha kupata mbolea.
Mbolea hiyo inatolewa kwa bei ya ruzuku ambapo mbolea inayouzwa sokoni kwa shilingi 136,000 wakulima wanapewa kwa shilingi 70,000 ikiwa na maana kuwa Serikali inachangia hizo gharama nyingine.
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mhandisi Magreth Kavalo amewataka Wakulima wote waliojiandikisha kwaajili ya kupata mbolea, kufika ofisi ya kilimo iliyopo Ngudu karibu na Kituo cha polisi ili wachukue mbolea na kwenda kuzitumia kama ilivyokusudiwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.