Mheshimiwa Dkt. Alice Kaijage Mbunge wa watumishi amefanya ziara Wilayani Kwimba leo Agosti 1,2024 ambapo amesikiliza kero na changamoto za wafanyakazi na amezitolea ufafanuzi huku changamoto nyingine akiahidi kuzifikisha katika wizara husika
" ni utaratibu wangu kama muwakilishi wa watumishi kusikiliza changamoto ili nikaziwasilishe mahali husika kwaajili ya kupatiwa ufumbuzi"
Katika kikao hicho Dkt Kaijage ameeleza namna Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anavyoshughulikia changamoto za watumishi ikiwa ni pamoja na kupandisha madaraja, ajira za kada mbalimbali.
Aidha Kaijage ametumia wasaa huo kuhamasisha watumishi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura
" viongozi hawa wenyeviti wa vijiji na mitaa wana maana sana kwenye jamii tunazoishi sasa ili tupate viongozi tunaowapenda lazima tujiandikishe ili wakati ukifika tuweze kuwachagua, jitahidini mjiandikishe ili uchaguzi ukifika muweze kupiga kura" amesema Kaijage
Akiwasilisha taarifa ya Halmashauri Bi. Happiness Msanga Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba amesema changamoto za watumishi wengi zimeendelea kutatuliwa ikiwa ni pamoja kupandishwa madaraja, kulipa malimbikizo ya mishahara na kulipa fedha za kujikimu kwa watumishi walioajiliwa hivi karibuni
Watumishi walioshiriki kikao hicho wamemshukuru kiongozi huyo na wameshauri utaratibu huo uwe endelevu ili changamoto za watumishi zipatiwe ufumbuzi kwa wakati
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.