Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija ameendelea na ziara ya Kata hadi Kata kusikiliza malalamiko na kero za wananchi ambapo Leo Septemba 29,2023 amesikiliza kero za wananchi wa Kata ya Malya na Nkalalo.
Katika ziara hiyo kero zilizojitokeza ni uhaba wa maji, umeme kukatika katika, Barabara kutokarabatiwa kwa wakati na mgogoro wa wafanyabiashara, wamiliki wa vibanda vya stendi ya Malya na Halmashauri
Mkuu wa Wilaya amewataka wafanyabiashara kutii Sheria bila shuruti vilevile amesisitiza kuwa vibanda vilivyojengwa eneo la Halmashauri ni mali ya Serikali hivyo wapangaji wa vibanda hivyo wanatakiwa kulipa Kodi kama Halmashauri inavyoelekeza.
Aidha katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ametatua changamoto ya upatikanaji wa maji Kata ya Malya ambapo amewataka RUWASA kuhakikisha wanatengeneza miundombinu iliyoharibika haraka
" naelekeza kufikia jumatatu maji yawe yameshaanza kutoka, tengenezeni hizo mashine zilizoharibika watu wapate maji" Ludigija
Mheshimiwa Ludigija ameitumia ziara hiyo kuwataka wafanyabiashara wa nyama kuhakikisha bei ya nyama haizidi elfu Saba kwa kilo moja.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.