Mhe.Selemani Jaffo (MB), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) ametoa pongezi zake kwa uongozi wa Halmashauiri ya Wilaya ya Kwimba kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa jengo la Upasuaji, Wodi ya akinamama, Maabara, Chumba cha kuhifadhia maiti na Nyumba moja ya mtumishi katika ujenzi wa kituo hicho.
“Kituo hiki cha kutolea huduma Malya kwa moyo wangu wa dhati mmekitendea haki sana”
Hayo aliyasema Mhe. Jaffo wakati wa ziara ya kutembelea kituo hicho tarehe 05 /07/ 2018 Wilayani Kwimba.
Mhe.Selemani Jaffo akiongea na wananchi wa kata ya Malya.
Mhe. Jaffo alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. John Pombe Magufuli kwa moyo alionao wa kuwatumikia watanzani katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya.
“Mhe Rais hatawaangusha katika kipindi chake cha uongozi, anahakikisha fedha zote zinazowahusu watanzania zinawafikia pamoja na miradi iliyosimama kwa mda mrefu inakamilika,”
Pamoja na kumpongeza Rais, Mhe. Jaffo amewataka wananchi wa kata ya malya kuhakikisha wanajiunga na Mfuko wa Jamii (CHF) iliyoboreshwa kwa ajili ya kupunguza gharama za matibabu.
Aidha Mhe. Jaffo amemtaka Mganga Mkuu wa Wilaya Dr.Elias Misana kuhakikisha kituo cha afya Malya kinafungwa mfumo wa utoaji taarifa za ukusanyaji wa mapato ya hospitali (GHOMIS).
Mhe.Selemani Jaffo akiweka jiwe la msingi katika mradi wa Ujenzi wa kituo cha kutolea huduma za afya Malya.
Kwa kuongezea Mhe. Jaffo amemuagiza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Dr. Zainabu Chaula kuhakikisha anatenga fedha maalum kwa ajili ya ujenzi wa jengo maalum la “Utrasound” na “Exray” Mashine kwa lengo la kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.
Naye Mbunge wa Jimbo la Sumve Mhe. Richard Ndassa amezishukuru kamati zote kwa moyo wa kujitolea usiku na mchana ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa kiwango kilichokusudiwa pamoja na kufuata maagizo waliokuwa wanapewa na wataalam kutoka Wilayani.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon amesema changamoto kubwa inayovikumba vituo vya kutolea huduma ni pamoja na upungufu wa watumishi hivyo basi amemuomba Mhe. Jaffo kuhakikisha kituo cha afya Malya kinapata watumishi wa kutosha ili kiweze kufanya kazi iliyodhamiliwa na hatimaye wananchi waweze kufurahia maendeleo ya nchi yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ilipokea jumla ya shillingi millioni 400,000,000/= kwa ajili ya ujenzi i wa kituo hicho kwa lengo la kutekeleza mkakati wa serikali wa kuviboresha na kujenga vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili viweze kutoa huduma bora inayoendana na mahitaji halisi ya wananchi.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.