Mbunge vitimaalumu wanawake Mkoa wa Mwanza Mhe.Kemilembe Lwota amekabidhi milioni 10 kwa shule ya Sekondari Tallo ikiwa nijuhudi za kuunga mkono ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kidato cha tano, pesa hizo zimepokelewa na Mwenyekiti wa bodi ya shule Ndug.Ramadhani Kasara na Mkuu wa shule Mwlm.Fadhili Yusufu katika ukumbi wa Halmashauri ya Kwimba leo tarehe 12 Juni 2020.
Akikabidhi mchango huo Mhe.Kemilembe amewataka viongozi wa shule hiyo kuzitumia fedha hizo kukamilisha bweni moja ambalo liko kwenye hatua za ukamilishaji,bweni hilo likikamilika litaweza kuchukua wanafunzi 100. Shule ya Sekondari Tallo inatarajia kuanzisha masomo ya kidato cha tano na sita kwa michepuo ya HGE na EGM.
Katika zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kwimba Bib.Pendo Malabeja,Afisa Elimu Sekondari Mwlm.Emmanuel Katemi na Mwenyekiti wa bodi ya Shule wamemshukuru Mhe.Kemilembe kwa pesa hizo kwani zitasaidia kumalizia jengo hilo na wameahidi kusimamia pesa hizo ili zifanye kazi kama iliyokusudiwa ili jengo likamilike kwa wakati.
Miundombinu mingine inayohitajika kwa ajili ya kidato cha tano katika shule hiyo imeshakamilika ambayo ni bweni moja,bwalo,madarasa mawili na choo cha wanafunzi na Walimu.Shule hiyo ikikamilika itaongeza idadi ya shule za kidato cha tano na sita ambazo kwa sasa ziko 3.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.