Kabla ya tarehe 23/04/2021 mtandao utapatikana 'Kundo'
Naibu Waziri wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mhe. Kundo Andrea amewaahidi wananchi wa kata ya Bugando Wilayani Kwimba kuwatatulia changamoto ya Mawasiliano.
Mhe.Kundo ameyasema hayo kwenye ziara yake ya kukagua minara na kubaini changamoto za mawasiliano katika Wilaya ya Kwimba leo tarehe 08/01/2021,ambapo amebaini tatizo la upatikanaji wa mtandao hapo akaahidi kutatua changamoto hiyo,vilevile amesema minara mitano inatarajiwa kujengwa ili kuondoa kabisa tatizo la kukosekana kwa mtandao katika Kata zisizopata mtandao.
Mhe.Kundo amewataka viongozi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mitandao na amewataka wananchi kutobagua mitandao bali watumie mtandao unaopatikana kwa urahisi.
Aidha Mhe. Kundo ameyataka makampuni ya mitandao ya TTCL,Vodacom,Tigo,Halotel na Airtel kufanya utafiti ili kujua maeneo ambayo hakuna mtandao ili wakaboreshe upatikanaji wa mtandao hasa intaneti(internet).
Katika ziara hiyo Mhe.Kasalali Mageni Mbunge wa Sumve amemshukuru Naibu Waziri kwa ujio wake na ameahidi kufanyia kazi maelekezo na ushauri alioupata.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.