Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella akimkabidhi mkuu wa wilaya ya kwimba Mhe. Bi Senyi Simon Ngaga Mwenge wa Uhuru tayari kwa uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kwimba.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika kijiji cha Izizimba A katika wilaya Kwimba tarehe 26/08/2018 tayari kwa kuanza kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi saba (7) ya maendeleo ambayo imechangiwa kwa nguvu za wananchi kwa michango mbalimbali pamoja na fedha kutoka Serikalini. Mhe Mkuu wa Wilaya bibi. Senyi Simon Ngaga amesema kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2018 zinaongozwa na Ndg. Charles Francis Kabeho ambaye ni kiongozi mkuu wa mbio za Mwenge Kitaifa na utakimbizwa zaidi ya kata nne huku ukipita zaidi ya kilometa 119 katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kwimba . Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa katika wilaya ya Magu mapema tarehe 27 mwezi Augost mwaka huu tayari kwa kupitia na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na shughuli nyingine.
Ndg. Charles Francis Kabeho akizungumza na wananchi na kuhamasisha elimu bure
Ndg. Charles Francis Kabeho ambea ndiye kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2018 amesema kuwa wazazi wanao wajibu wa kuwaandikisha watoto, kuwapeleka shule na kuchangia chakula shuleni ili kuongeza afya ya watoto wakiwepo shuleni ili kupunguza utoro na kuongeza ubora wa elimu kulingana na kauli mbiu ya Mwenge mwaka huu isemayo “Elimu ni Ufunguo wa Maisha wekeza sasa kwa Maendeleo ya Taifa”. Wazazi watupie jicho suala la maendeleo ya watoto wao kielimu kwa kuwasisitiza kuwa kujisomea shuleni na nyumbani ili kupata elimu bora ukizingatia mfumo wa elimu bure unaotolewa na serikari ya awamu ya tano bila kujali ni tabaka lolote. Pia Ndg. Charles Kabeho ameongeza kuwa mkoa Mwanza ni mkoa wa 26 kati ya mikoa 31 itakayopitiwa na mbio hizi. Mwenge wa uhuru ulianza mbio zake mnamo April 02 mwaka huu mkoani Geita na utahitimisha mbio zake mkoani Tanga October 14 2018 ambapo ni siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julias K Nyerere.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.