Naibu Waziri Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. David Silinde amefanya ziara ya kikazi tarehe 07 /03/2021 Wilayani Kwimba, kukagua ujenzi wa miradi ya EP4R katika Shule ya Sekondari Tallo,
Mhe.Silinde ametembelea Shule hiyo na kukagua ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kidato cha tano,ujenzi wa madarasa mawili na ujenzi wa matundu sita ya vyoo unaoendelea,ambapo madarasa na matundu ya vyoo yameshakamirika na bweni liko kwenye hatua za ukamilishaji.
Shule ya Sekondari Tallo imefanikiwa kupata miradi ya EP4R kwa miaka mitatu mfurulizo ambapo mwaka wa fedha 2017/2018 Shule ilipokea milion 81.6 kwa ajili ya ujenzi wa Bweni na Matundu sita ya vyoo ambayo yameshakamilika, mwaka 2018/2019 Shule ilipokea milioni 175 kwaajili ya ujenzi wa Bweni moja,ukamilishaji wa Bwalo moja,ujenzi wa jiko,ujenzi madarsa mawili na ujenzi wa matundu nane ya vyoo vyote vimekamilika. Mwaka 2020/2021 Shule ilipokea milioni 126.6 kwaajili ya ujenzi wa Bweni moja,ujenzi wa madarasa mawili na ujenzi wa matundu sita ya vyoo. ambapo miradi yote hii imelenga kutoa Elimu ya kidato cha tano na sita katika Mazingira mazuri yanayohamasisha ufundishaji na ujifunzaji.
Mwaka 2020 Shule ya Sekondari Tallo iliweza kuanzisha masomo ya kidato cha Tano baada ya maandalizi ya kupokea wanafunzi hao kukamilika, jumla ya wanafunzi 64 wanasoma kidato cha Tano na maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wengine yanaendelea.
Aidha Mhe.Silinde amesisitiza majengo hayo kukamilika kwa wakati ili malengo ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli yakutoa Elimu katika mazingira bora yatimie.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.